Breaking News

Sunday, December 10, 2017

ZLSC YAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu  Bw. Mohammed  Khamis akiwasilisha mada ya Dhana ya Haki za Binadamu katika Maadhisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Kijangwani mjini Unguja.  Kushoto ni Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Bw. Haji Abdalla Haji na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa ZLSC Bi Saida Amour Abdalla

Washiriki wakisiliza mada ya Haki za Binadamu katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja

Mshiriki akichangia mada

Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Mjini Mgharibi Bw. Haji Abdalla Haji  ( aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi  wa ZLSC, Wafanyakazi, na Wadau wengine baada ya  maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika Kijangwani mjini Unguja. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Bw. Mohammed Khamis na  kushoto ni  Mjumbe wa Bodi wa ZLSC Bi. Salma Saadati  

Read more ...

Wednesday, December 6, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR CHAADHIMISHA MIAKA 25

Tarehe 2 Disemba 2017, Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kiliadhimisha miaka 25  tokea kuanzishwa  kwake   sambamba  na kumbukizi ya  muasisi wa Kituo Marehemu Profesa Haroub Othman, iliyofanyika ukumbi wa  Baraza la Wawakilishi  la zamani, Kikwajuni  mjini Unguja.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji  Ussi (Gavu)  ambaye alikipongeza Kituo kwa kuweza kufikisha miaka 25.

Maadhimisho hayo pia yalifuatiwa na uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar  pamoja na kutolewa zawadi kwa waanzilishi wa Kituo na Wajumbe wa Bodi waliotangulia.
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kumbukizi ya Muasisi wa Kituo Marehemu Prof. Haroub Othman

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji  Ussi (Gavu) akizindua kitabu cha Miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, katika maadhimisho yaliyofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni mjini Unguja,  (kati kati)  Kaimu Mkurugenzi wa  Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,  akifuatiwa na Afisa Mipango Bi. Moza Kawambwa Nzole

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji Ussi (Gavu) akionesha kitabu cha Miaka 25 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, baada ya kukizindua (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi wa  Kituo Prof. Chris Maina Peter

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa Haji  Ussi (Gavu)  akimkabidhi zawadi muanzilishi na  aliyekuwa Mjumbe wa Bodi  wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,  Bi. Fatma Maghimbi
Read more ...

Sunday, December 3, 2017

KUMBUKIZI YA MAREHEHEMU PROFESA HAROUB OTHMAN

Wanafunzi wakimuombea dua Muasisi wa Kituo cha  Huduma za Sheria
Zanzibar,
 Marehemu Prof. Haroub Othman

Wanafunzi wakisoma dua  

Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar wakijumuika na
wanafunzi katika kumuombea dua muasisi  wao. Mungu ailaze
roho ya Marehemu  mahala pema peponi. AMIN 

Read more ...

Thursday, November 23, 2017

MAFUNZO YA KUWAKUMBUSHIA MRADI WA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA KWA MAAFISA WA CHUO CHA MAFUNZO

Baadhi ya Maafisa Polisi  wa  Chuo cha Mafunzo, wakiwa katika mafunzo ya kukumbushwa juu ya Mradi wa Watoto Wanaokinzana na Sheria, yaliyoandaliwa   na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar

Read more ...

Friday, November 3, 2017

BALOZI WA UFARANSA AMETEMBELEA ZLSC

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kimetembelewa na Balozi wa Ufaransa Bi Malika BERAK kwa lengo la kutaka kujua shughuli mbali mbali zinazofanywa na Kituo.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi Saida Amour Abdalla, akimfafanulia Balozi wa Ufaransa Bi. Malika BERAK kazi za Kituo

Read more ...

Thursday, October 26, 2017

MKUTANO WA MWAKA KWA WADAU WA KITUO (ZLSC)

Kaimu Mkurugenzi Wa Kituo Cha Huduma Za Sheria Zanziabar
Bi Saida Amour akiwasilisha taarifa ya kazi za Kituo kwa mwaka
2017,katika Mkutano hou.
Mmoja wa washidau wa Kituo Bi Suzani Kunambi akichangia
 mada  baada ya kupokea taarifa ya kazi zilizofanywa na
Kituo kwa mwaka
2017.Read more ...

Tuesday, October 24, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KIMEFANYA MAFUNZO YA WASAIDIZI WA SHERIA KWA JUMUIYA YA ZAWOPA(Zanzibar Women Paralegal)


Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kimeandaa  mafunzo ya siku mbili kwa  Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Wanawake  (ZAWOPA).  Mada mbali mbali  ziliwasilishwa ambazo ni Ndoa na Talaka, Malezi Bora, Matunzo na Ukaazi wa Mtoto kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto, Dhana ya Ugatuzi, Sheria ya Mahakama ya Ardhi pamoja na Rushwa na Changamoto katika Ardhi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo tarehe 24 na kumaliza kesho tarehe 25 Oktoba 2017 kwa lengo la kutoa uelewa juu masuala mbali mbali ya kijamii na kuendelea kuwajengea uwezo Wasaidizi wa Sheria waliokwisha hitimu mafunzo yao.


Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma Zanibar
 Bi. Saida Amour Abdalla akifafanua aina za talaka
                                 


Wasaidizi wa Sheria wakifanya kazi za vikundi Msaidizi wa Sheria akiwasilisha  kazi ya kikundi


Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen