Breaking News

Friday, October 20, 2017

ZIARA YA KLABU YA ELIMU YA URAIA KWA WANAFUNZI

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kikiwasili katika moja ya  zilizotembelewa ambayo ni skuli ya sekondari Jumbi kwa lengo la kukagua klabu ya wanafunzi skulini hapo. 

Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Ali Haji Hassan akiwa na watoto waliopelekwa skuli  na walimu  wa skuli ya Jumbi baada ya watoto hao kukosa  haki ya  elimu bila sababu za msingi na umri ukiwa umesonga ,  Haya ni matunda ya ZLSC baada ya kuwapatia  elimu ya uraia walimu  wa skuli mbali mbali 

Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw Mohammed Kh. Mohammed wa (kwanza kushoto) na Bw. Ali Haji Hassan (wa kwanza kulia)   wakiwa na Afisa elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  Bw. Daudi Suhuba  ( alievaa suti ya kijijvu jivu) pamoja na  walimu wa skuli ya Paje, katika  wakizungumzia maendeleo ya klabu  walipofika skulini hapo kukagua klabu hiyo

Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Ndijani waliojiunga na Klabu ya Elimu ya uraia wakimsikiliza Afisa Mipango  Bw. Ali Haji Hassan ( hayupo pichani) 

Wanafunzi wa  klabu ya skuli ya Paje wakifanya igizo la Udhalilishaji

Read more ...

ZLSC YAFANYA KONGAMANO LA SIKU YA ADHABU YA KIFO DUNIANI

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kiliungana na Mataifa mengine duniani kufanya  kongamano la siku ya kupinga Adhabu ya Kifo Duniani ambayo kikawaida hufanyika kila ifikapo tarehe 10.10 kila mwaka.

Kwa mwaka 2017 maadhimisho hayo yalifanyika  kijiji cha Uvivini, kisiwani Tumbatu  kwa Unguja na Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake  kwa Pemba.

Lengo la kongamano hilo ni kukutana na Wadau mbali mbali kwa ajili ya kuelezea hali halisi ya utekelezaji wa hukumu ya kifo na kukusanya maoni.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "UMASIKINI ISIWE SABABU YA KUHUKUMIWA KIFO"Washiriki wa Kongamano la siku ya kimataifa ya kupinga Adhabu ya Kifo wakiwa safarini kuelekea  kijiji cha Uvivini kisiwani Tumbatu, kwa ajili ya maadhimisho 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar  Prof. Chris Maina Peter ,akitoa ufafanuzi  wa  adhabu ya Kifo kwa  wananchi wa kijiji cha Uvivini kisiwani Tumbatu, katika kongamano la siku ya kimataifa  la kupinga Adhabu ya Kifo Duniani

Mratibu   wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,  Ofisi ya Pemba Bi. Fatma Khamis Hemed, akiwakaribisha washiriki wa Kongamano la Siku ya kimataifa la kupinga adhabu ya kifo lilifanyika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake Pemba   

Washiriki wa Kongamano  wakisiliza kwa makini mada  inayotolewa, katika Kongamano lilifanyika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Chake Chake Pemba

Read more ...

Thursday, October 5, 2017

MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU KWA WATU WALIOATHIRIKA NA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA YALIYOFANYIKA TAREHE 05 OKTOBA 2017

Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Bw. Thabit Abdulla Juma akitoa mada ya Haki za Binadamu kwa watu walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya, katika mafunzo yaliyofanyika  ZLSC Kijangwani , mjini -Unguja, tarehe 05 Oktoba 2017

Read more ...

ZIARA YA WANAFUNZI WA SKULI YA SEKONDARI KWARARA KWA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR

Mwanafunzi wa skuli ya Sekondari Kwarara akielezea  mafunzo aliyoyapata baada ya kuja kituoni katika ziara ya kukitembelea Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kilichopo Kijangwani mjini Unguja,  ziara hiyo ilifanyika tarehe 03 Oktoba 2017

Read more ...

Wednesday, September 13, 2017

MAFUNZO KWA MASHEHA NA DIWANI WA WILAYA YA KATI

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kimeandaa mafunzo kwa Masheha wa Wilaya ya Kati  yaliyofanyika  katika Ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja, tarehe 13 Septemba 2017
Lengo la mafunzo hayo ni kuwatambulisha Wasaidizi wa Sheria kwa Masheha na kuwataka  Masheha,  kuwatumia Wasaidizi wa Sheria na   kushirikiana nao katika kutetea  na kuzilinda haki za binadamu.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,  Bi.Saida Amour Abdallah akifungua mafunzo  kwa Masheha  wa Wilaya ya Kati Unguja, yaliyofanyika tarehe 13 Septemba 2017  Kijangwani mjini Unguja

Afisa Mipango wa ZLSC Bi Moza Kawambwa Nzole akiwasilisha mada ya dhana ya Wasaidizi wa Sheria  kwa washiriki wa mafunzo  kwa  Masheha wa Wilaya ya kati
Read more ...

Tuesday, September 12, 2017

MAFUNZO YA WAZAZI JUU YA MALEZI SALAMA NA MASHIRIKIANO YA BABA

Kituo cha  Huduma za Sheria Zanzibar, kimefanya mafunzo kwa wazazi juu ya malezi salama na mashirikiano ya baba, yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalikuwa na lengo la kuwashirikisha baba katika malezi ya watoto (Male Engagement on Positive Parenting) kutokana na baba wengi kuwaachia jukumu  akina mama na kusahau wajibu wao.
Kupitia mafunzo hayo wanaume walipata elimu ya kutosha juu ya namna ya kushirikiana na wanawake  katika malezi ili kuhakikisha watoto wanapata malezi bora na salama.
Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza tarehe 10 Septemba 2017 na kumalizika tarehe 12 Septemba 2017.

Wazazi  wakiwa katika mafunzo ya malezi salama na mashirikiano ya baba, yaliyofanyika katika Ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja, tarehe 12 Septemba 2017
Read more ...

Monday, August 14, 2017

ZLSC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WA BARAZA LA VIJANA KWA MKOA WA KUSINI UNGUJA JUU YA ELIMU YA URAIA

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar,  Bi Saida Amour Abdalla, akifungua mafunzo  kwa Vijana wa Baraza la Vijana kwa Mkoa wa Kusini Unguja, yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC,  Kijangwani mjini Unguja, tarehe 14 Agosti, 2017 

Read more ...

Friday, August 11, 2017

TATHMINI YA KUJADILI MPANGOKAZI WA KITUO WA MWAKA 2013/2017


 Wadhamini, Wafanya tathmini, Wajumbe wa Bodi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, wafanyakazi na wadau wengine, wakiwa katika kikao cha tathmin ya kujadili mpango kazi wa Kituo,  uliofanyika katika ukumbi wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) mjini Unguja tarehe  11 August 2017
Read more ...

Wednesday, August 9, 2017

ZLSC YATOA MAFUNZO KWA VIJANA WA BARAZA LA VIJANA KWA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA JUU YA ELIMU YA URAIA YALIYOFANYIKA

KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar chatoa mafunzo ya elimu ya uraia kwa vijana wa  baraza la vijana kwa Mkoa wa Kaskazini,  Unguja.
Mfunzo hayo yalifanyika  katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani tarehe 09 Agosti 2017   kwa lengo la kutoa uelewa wa elimu ya uraia kwa vijana.


Washiriki wakiwa katika mafunzo ya elimu ya uraia kwa vijana wa Baraza la vijana  kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja  yaliyofanyika katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani tarehe 09 Agosti 2017

Read more ...

MAFUNZO YA KUWATAMBULISHA WASAIDIZI WA SHERIA KWA WATUMISHI WA IDARA MAALUM (VIKOSI) SMZ


Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kimefanya mafunzo ya kuwatambulisha Wasaidizi wa Sheria kwa Watumishi wa Idara maalum (Vikosi) vya SMZ. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa ZLSC kijangwani Mjini Unguja tarehe  09 Agosti 2017 kwa lengo la kutoa uelewa wa sheria kwa  watumishi hao.

Akizungumza katika mafunzo hayo, mratibu  ambae ni Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi Moza   Nzole aliwataka watumishi hao kufuata haki na sheria katika utendaji wao ili kuwafanya raia wawe na imani juu ya vikosi hivyo.


Washiriki wakiwa katika mafunzo ya kuwatambulisha Wasaidizi wa Sheria kwa watumishi wa Idara Maalu ( vikosi) SMZ yaliyofanyika  katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja tarehe 09 Agosti 2017 

Read more ...

Monday, August 7, 2017

MKUTANO WA NUSU MWAKA KWA WASAIDIZI WA SHERIA


Mratibu wa Mafunzo ya wasaidizi wa sheria  Bi  Moza Nzole akiwa katika Mkutano wa nusu mwaka kwa wasaidizi wa sheria kujadili matarajio, mwelekeo mapungufu pamoja na changamoto za mradi wa wasaidizi wa sheria Zanzibar uliofanyika tarehe 07 August 2017 katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mijini Unguja
Read more ...

MAFUNZO YA USHIRIKISHWAJI WANANCHI KATIKA UTAYARISHAJI WA KATIBA NA SHERIA


KITUO  cha Huduma za Sheria Zanzibar kimetoa
mafunzo kwa viongozi wa dini na watendaji wa
Serikali za Mitaa kuhusu Ushirikishwaji wananchi
katika utayarishaji Katiba na Sheria.

Mafunzo hayo yalifanyika Tarehe  07 Agosti 2017
katika ukumbi wa Kituo  Kijangwani mjini Unguja
kwa lengo la kuwajengea uwezo wa namna Sheria
na Katiba zinavotayarishwa


Mratibu wa mafunzo ambae ni Afisa Mipango wa
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw Ali Haji
Hassan akiwasilisha mada ya namna ya ushirikishwaji
wananchi katika utayarishaji Katiba na Sheria  katika
mafunzo yaliyofanyika  ZLSC Kijangwani
yaliyowajumuisha viongozi wa dini na watendaji wa
serikali za mitaa
Read more ...

Wednesday, July 26, 2017

Afisa Mipango Bw. Thabit Abdula kutoka kituo Cha Huduma za
Sheria zanzibar (ZLSC) akitoa mada katika mafunzoya vijana
 kwa baraza la vijana la Mkoa wa mjini Magharib yaliyofanyika
katika Ukumbi wa mikutano wa Kituo (ZLSC) tarehe 26/07/2017

Add caption


Read more ...

Monday, July 24, 2017

MAFUNZO YA WASAIDIZI WA SHERIA (PARALEGALS)

Dokta Yahya (aliyesimama) ambaye ni mmoja wa walimu
aliyekuwa akitoa mada katika Mafunzo ya Wasaidizi wa Sheria
yaliyofanyika tarehe 22 na 23/07/2017 Katika ukumbi wa
mikutano Kituoni (ZLSC) Zanzibar


Wasaidizi wa Sheria  wakiwa makini kumsikiliza mmoja wa
Walimu aliyekuwa akiwasilisha mada katika Mafunzo hayo
Read more ...

Wednesday, June 21, 2017

ZLSC YAFANYA MKUTANO WA WADAU KUHUSIANA NA UTAFITI WA VURUGU ELEKEZI

Afisa Mipango wa Kituo Cha Huduma za Sheria Zanzibar akiwasilisha mada juu ya Vurugu Elekezi   katika mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria ,  Kijangwani Mjini Unguja  tarehe 21 Juni 2017

Kituo kwa kushirikiana na Shirika la PILPG, pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na UtawalaBora
Tanzania (CHRAGG) na LHRC kinafanya tafiti juu ya vurugu elekezi (Violent Extremism).

Katika kulifika hili Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilianadaa mkutano maalum  kwa kuwahusisha wadau mbali mbali wakiwemo  Jeshi la Polisi, Chuo cha Mafunzo, DPP  na Mahakama uliofanyika tarehe  Juni 21, 2017 katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja.

Lengo kuu la utafiti huu ni kuangalia mtizamo wa juu kuhusiana na vyombo vinavyohusika na utoaji haki kwa upande wa Zanzibar pamoja na kuangalia njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo.

 Akizungumza katika mkutano huo Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Ali Haji Hassan alisema , Vurugu elekezi ni kitendo cha kutumia nguvu, kutumia vurugu, au kuhamasisha watu wengine kutumia nguvu au vurugu, ili kufikia malengo fulani ama ya kiitikadi, kidini, kisiasa kijamii au hata kiuchumi.

Washiriki katika mkutano wakichangia mada walisema kuwa ili kulitatua tatizo hili ni vyema jamii ikapewa elimu ya kutosha  kwa watu wa rika zote.
Waliitaka jamii ishikamane pamoja kama meno ya vitana ili kuondosha tatizo hili na kupata nchi njema yenye maendeleo endelevu.


Afisa Mipango wa ZLSC akiwasilisha mada kwa wadau mbali mbali 

Msaidizi wa  Sheria kutoka Muyuni akichangia mada Read more ...

Thursday, June 15, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR CHAFANYA UZINDUZI WA RIPOTI YA 11 YA HAKI ZA BINADAMU

Mgeni Rasmi Mhe. Mshibe Ali Bakari  wa pili kulia  akiwa katika uzinduzi wa Ripoti ya 11 ya Haki za Binadamu iliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar  tarehe 15/06/2017. 

Mgeni Rasmi Mhe. Mshibe Ali Bakari akiwa na wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar DPP na  Kaimu Mkurugenzi wakionesha kitabu kilichozinduliwa.

 Mgeni rasmi Mhe. Mshibe Ali Bakari akiwa katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa Bodi , DPP , Kaimu Mkurugenzi na baadhi ya Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar baada ya uzinduzi kukamilika.

Read more ...

Sunday, April 9, 2017

MAHAFALI YA NNE YA WASAIDIZI WA SHERIA YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA KIJANGWANI-ZANZIBAR TAREHE 08/09 APRILI 2017

Mhe Mgeni Rasmi ,Waziri wa Katiba na Sheria, Utumishi wa  Umma na Utawala Bora, Zanzibar . Haroun Ali Suleiman (katikati)  akifuatilia kwa makini  kikundi cha Sanaa cha Thesode  katika mahafali ya Nne ya Wasaidizi wa sheria yaliyofanyika Tarehe 09 Aprili 2017,  Katika Ukumbi wa Kituo Cha Huduma na Sheria -Kijangwani Zanzibar kulia ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini Profesa Maina Peter akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Bi Saida Amour, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi   
Wasanii wa ngoma za Kibati  wakitumbuiza katika mahafali ya nne ya Wasaidizi wa Sheria


Washiriki kutoka sehemu mbali mbali Ikiwemo , Kenya, Tanzania  Bara, Pemba na Unguja , waakiwemo na Wafanya kazi wa Kituo Cha Huduma za Sheria Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi( hayupo pichani) 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Profesa Chris Maina Peter, akimkaribisha Mgeni Rasmi,  Waziri wa Katiba na Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman katika Mahafali ya nne ya Wasaidizi wa Sheria . 

Read more ...

Saturday, March 11, 2017

MAFUNZO YA HAKI ZA BINAADAMU KWA WAANDISHI WA HABARI YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA ZLSC KIJANGWANI ZANZIBAR TAREHE 11\03\2017


 Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa
ZLSC  kusubiria mafunzo ya Haki Za Binaadamu..

Afisa Mipango  Thabit Abdullah kutoka Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar (ZLSC)   akiwasilisha mada ya Haki za
Binaadamu na nafasi ya Waandishi wa habari kwa jamii. 
Mwanasheria   Rashid Abdallah akiwasilisha mada ya
Madhara ya Rushwa katika usimamizi wa Haki za Binaadamu.


Mshauri wa vyombo vya Habari  Salim Said Salim akiwasilisha
 mada  kuhusu kanuni, miiko na maadili ya Waandishi wa
Habari Kitaifa na Kimataifa.

Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini mada
zinazowasilishwa katika mafunzo hayo.
Read more ...

Wednesday, March 8, 2017

MAAZIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KIJANGWANI TAREHE 7/03/2017

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR,  RIZIKI PEMBE JUMA AKITOA HOTUBA YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kimataifa  kila mwaka ifikapo Terehe 8 Machi, lengo kuu ni kumuendeleza mwanamke kiuchumi, kijamii, na  kisiasa ili kumpa fursa ya  kuwa na maendeleleo endelevu.

 Kwa kuzinagatia hilo Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na Asasi tofauti zisizo za kiserikali  ambazo ni ZAFELA, TAMWA, ZGC, SOS, Action Aid na Save New Generation, wamekuwa mstari wa mbele katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani ambapo Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, na kauli mbiu  ya mwaka huu ilikua"Imarisha fursa za ajira kwa kumuezesha mwanamke kiuchumi" .

Siku ya wanawake duniani ilianza mwanzoni mwa  mwaka 1900's kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kuandamana kwa kupiga vita udhalilishaji na ukandamizwaji uliokuwa ukitokea katika maeneo ya kazi yakiwemo mazingira magumu na hatari,,ukosefu wa huduma za jamii pamoja na unyanyasaji,  .

Kuna mikakati mbali mbali inachukuliwa  ili kumuinua mwanamke katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii, ikiwemo kuundwa kwa tume mfano TAMWA. Kuwepo kwa dawati la jinsia, wanawake na watoto, pamoja na kumuinua kielimu kwa kuwawekea skuli maalum mfano Benbella Girls Secondary School ili kuwakuza wanawake kifikra kwa lengo la kupata usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamme.


Jumla ya washiriki 50 walihudhuria maadhimisho hayo wakiwemo Wanaharakati wa Wa Haki za Binaadamu na masuala ya Kijinsia yaliyofanyika tarehe 07/03/2017 katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.

Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen