Breaking News

Friday, October 20, 2017

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR KILIFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KLABU ZA ELIMU YA URAIA KATIKA SKULI ZA MIKOA MITATU YA UNGUJA

Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kikiwasili katika moja ya  skuli ilizotembelea ambayo ni skuli ya sekondari Jumbi kwa lengo la kutembelea  klabu ya wanafunzi skulini hapo. 

Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Ali Haji Hassan akiwa na watoto waliopelekwa skuli  na walimu  wa skuli ya Jumbi baada ya watoto hao kukosa  haki ya  elimu bila sababu za msingi na umri ukiwa umesonga ,  Haya ni matunda ya ZLSC baada ya kuwapatia  elimu ya uraia walimu  wa skuli mbali mbali 

Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw Mohammed Kh. Mohammed wa (kwanza kushoto) na Bw. Ali Haji Hassan (wa kwanza kulia)   wakiwa na Afisa elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  Bw. Daudi Suhuba  ( alievaa suti ya kijijvu jivu) pamoja na  walimu wa skuli ya Paje,wakizungumzia maendeleo ya klabu  walipofika skulini hapo kutembelea klabu hiyo

Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Ndijani waliojiunga na Klabu ya Elimu ya uraia wakimsikiliza Afisa Mipango  Bw. Ali Haji Hassan ( hayupo pichani) 

Wanafunzi wa  klabu ya skuli ya Paje wakifanya igizo la Udhalilishaji
Wanafunzi wa Skuli ya Kombeni wakiimba wimbo wa  kutokomeza udhalilishaji

No comments:

Post a Comment

Designed By Published. Moonga Stephen