Breaking News

Monday, May 14, 2018

ZLSC YAFANYA MJADALA JUU YA KUMALIZIKA KWA MRADI WA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA

Wakili wa watoto kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bw. Thabit Abdulla Juma, akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria  kwa Askari Dawati walioshiriki mjadala huo, uliyofanyika  katika ukumbi wa ZLSC Kijangwani,  tarehe 10 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mjadala huo uliyofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 10 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mjadala huo uliyofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 10 Mei 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, Bi Harusi Miraji Mpatani, akifungua mjadala  kuhusu hatma ya Mradi wa Watoto wanaokinzana na Sheria  kwa Mahakimu na Waendesha Mashtaka, uliyofanyika Mazsons Hoteli  Shangani Unguja, tarehe 11Mei 2018
Mahakimu na Waendesha Mashtaka wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Harusi Miraji Mpatani (kati kati) akifungua mjadala  kuhusu hatma ya Mradi wa Watoto wanaokinzana na Sheria,  uliyofanyika Mazsons Hoteli  Shangani Unguja, tarehe 11Mei 2018
Read more ...

Wednesday, May 9, 2018

MKUTANO WA KUJADILI HATMA YA MRADI WA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA ULIYOFANYIKA TAREHE 5 NA 6 MEI 2018


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, akifafanua jambo  katika mkutano wa kujadili namna ya kuwasaidia watoto baada ya kumalizika kwa mradi wa watoto  wanaokinzana na Sheria. Mkutano huo ulifanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani mjini Unguja tarehe  5 Mei 2018. Kushoto ni  Wakili wa watoto Bi. Jamila Masoud Khamis akifuatiwa na Wakili Ahmed Moh'd Abdurrahman

Kituo  cha Huduma za Sheria Zanzibar kilifanya mkutano wa kujadili namna ya kuwasaidia watoto wakati   mradi wa watoto wanaokinzana na sheria ukikaribia  kufikia hatma yake.

Mradi huo ulikuwa ukiendeshwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kwa kushirikiana na UNICEF.

Washiriki wa Mkutano huo walikuwa ni Askari Magereza na Wasaidizi wa watoto ambapo walipendeza watoto waendelee kuwakilishwa mahkamani hata kama mradi utamalizika.

Mradi huo ulianza  2014 na utekelezwaji wake ulianza  tarehe 1 Julai 2015, ukiwa na lengo la kuwawakilisha watoto mahkamani na kuhakikisha wanapata haki zao  kama ilivyobainishwa katika Sheria   ya Mtoto Na 6/2011.

Sheria ya Mtoto Na. 6/2011 katika kifungu cha 43 (1) (e) (iii) kinafafanua haki ya mtoto kuwa na uwakilishi na usaidizi wa kisheria mahkamani.

Awali mradi huu ulikuwa ukiendeshwa kwa Mkoa  wa mjini magharibi pekee  na baadae uliendeshwa   kwa mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo kwa mwaka huu unafikia mwisho.


 Afisa mipango na Wakili  wa watoto kutoka ZLSC Bw. Thabit Abdulla Juma, akitoa maelezo mafupi juu ya Mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria kwa Askari Magereza, katika mkutano uliofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 5 Mei 2018
Washiriki wakimsikiliza Bw. Ahmed Moh'd Abdurrahman akielezea  changamoto za Mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria, katika mkutano uliofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 5 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mkutano, uliofanyika ZLSC Kijangwani tarehe 5 Mei 2018
Wasaidizi wa  watoto  wakiwa katika mkutano wa kujadili hatma ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria uliofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
 Mshiriki akichangia katika mkutano huo uliofanyika ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018


Wasaidizi wa  watoto  wakiwa katika mkutano wa kujadili hatma ya mradi wa watoto wanaokinzana na Sheria ukiofanyika ukumbi wa ZLSC Kijangwani, tarehe 6 Mei 2018
Read more ...
Designed By Published. Moonga Stephen